Song of Solomon 2:12-14


12 Maua yanatokea juu ya nchi;
majira ya kuimba yamewadia,
sauti za njiwa zinasikika
katika nchi yetu.

13 a bMtini unatunga matunda yake ya mwanzoni,
zabibu zinazochanua zaeneza harufu nzuri.
Inuka, njoo mpenzi wangu.
Mrembo wangu, tufuatane.”

Mpenzi


14 cHua wangu penye nyufa za majabali,
mafichoni pembezoni mwa mlima,
nionyeshe uso wako,
na niisikie sauti yako,
kwa maana sauti yako ni tamu,
na uso wako unapendeza.
Copyright information for SwhKC